Yanga yatamba kuifunga Platinum FC
Kocha wa Yanga, Mdachi Hans Pluijm amesema hawatabweteka na ushindi wa awali wa 5-1 dhidi ya Platinum FC ya Zimbabwe wakati timu yake inaondoka kesho kwenda
Bulawayo, Zimbabwe kwa ajili ya mechi yao ya marudiano ya Kombe la vilabu la Shirikisho Barani Afrika.Mechi hiyo ya marudiano itachezwa wikiendi hii.
Yanga ilishinda 5-1 katika mechi ya awali ikiwa uwanja wa nyumbani, jijini Dar es Salaam na inahitaji ushindi wa aina yoyote, droo au hata ikifungwa magoli yasiyozidi 4 ili isonge mbele kunusa hatua ya 16 bora.
Pluijm amesema mpira wa miguu hautabiriki, hivyo watacheza kwa kulinda goli na kushambulia ili kulinda ushindi wao wa aDar es Salaam na kupata magoli ya ugenini.
“Chochote kinaweza kutokea ila tumejiandaa na ushindi”,amesema Pluijm.
Tayari kuna taarifa kuwa mashabiki wapatao 40 wa Yanga wanaondoka Dar es Salaam kwa basi maalumu ili kwenda kuishangilia timu hiyo