Apewa Talaka kupitia facebook
Mwanaume mmoja amepewa talaka na mkewe kupitia mtandao wa Facebook.
Talaka hiyo ilitolewa baada ya mkewe kuenda mahakamani akidai kuwa haki zake za unyumba zimekiukwa na mumewe ambaye hataki kuonekana nyumbani.
Mwanamke huyo mkaazi wa jiji la Brooklyn alitaka ruhusa ya mahakama kubadilisha hali yake ya ndoa kuwa “single” kwenye Facebook.
Jaji wa mahakama hiyo ya rufaa ya Manhattan , Matthew Cooper aliamua kuwa mwanamke huyo muuguzi Ellanora Baidoo anaweza kumtaliki mumewe kupitia kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.
Baidoo, 26, “ameruhusiwa kutangaza talaka yake kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook kwa sababu ndio njia ya pekee ambaye anawasiliana na mumewe''.
Na mara moja wakili wake mwanamke huyo alituma ujumbe wa kibinafsi kwa Victor Sena Blood-Dzraku akimjulisha kuhusu talaka hiyo.
“Ilani hii itatumwa mara moja kwa wiki na wakili wa mwanamke huyo kwa kipindi cha majuma matatu hadi atakapojibu mumewe'' alisema jaji.
Wakili wake Baidoo,Andrew Spinnell alifurahia sana uamuzi huo
''inapaswa kutumia hii ni sheria mpya'' alisema Spinell.
Mteja wake alifunga ndoa na mshtakiwa Blood-Dzraku mwaka wa 2009, lakini ndoa ya ilisambaratika Blood-Dzraku alipokataa kata kata kuendelea mbele na sherehe za kitamaduni kuambatana na mila za Bi Baidoo.
Wawili hao ni raia wa Ghana.
Spinnell alisema kuwa kile alichotaka bi Baidoo ni sherehe itakayojumuisha jamii zote mbili ''
Bibi huyo amesema kuwa hataki kulipwa fidia yeyote kutoka kwa mumewe kwani japo walifunga ndoa mumewe alikataa kutimiza tendo la ndoa naye.
Aidha majaribio kadha ya kuwapatanisha wawili hao imeambulia patupu huku ikibainika kuwa bwana Blood-Dzraku hataki kutoa talaka.
Kulingana na wakili huyo bwana huyo hajajibu ujumbe huo wa talaka.