Ja Rule,Pesa nyingi,nafasi nzuri kwenye filamu kubwa,mpaka leo anajuta kukata.
Muongozaji wa filamu za “2 Fast 2 Furious” John Singleton amezungumzia jinsi Ja Rule alivyokataa kulipwa nusu ya dola milioni moja ilikufanya filamu hio.
2 Fast 2 Furious imetajwa kuwa filamu kubwa zaidi inayohusu magari na maisha ya watu na muongozaji huyo amesema Ja Rule alijiskia mkubwa sana wakati huo ndio maana alikata nafasi hio.
John Singleton anasema baada ya Ja Rule kuringa ndio nafasi akapewa rapa Ludaris na ameitendea haki sana nafasi hio. John anasema alikutana na Ja Rule miaka kadha baadae na nikamwambia nikimpigia simu tena asidharau ofa zangu na yeye aliomba msamaha, sasa tuko sawa. Ja Rule aliigiza kwenye filamu ya kwanza ya Fast and the Furious.