Kim Jong-Un aahirisha ziara ya Urusi
Urusi imethibitisha kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un amefutilia mbali ziara yake mjini Moscow ambapo alipangiwa kushiriki maadhimisho ya ushindi katika vita kuu ya pili duniani wiki ijayo.
Ingekua ziara ya kwanza ya kiongozi huyo nje ya nchi yake tangu kuchukua hatamu za uongozi miaka mitatu iliyopita.
Ikulu ya Urusi Kremlin imesema kiongozi huyo ameamua kusalia Pyongyang kushughulikia masuala ya nyumbani.
Mabadiliko haya yamechochea tetesi kwamba huenda kiongozi kuyo wa Korea Kaskazini anakabiliwa na matatizo ya kisiasa nyumbani.