Kim Kardashian Kutozaa Tena


Mwanamitindo na muigizaji maarufu nchini marekani Kim Kardishian huenda asizae tena maishani mwake kutokana na tatizo la mfuko wa uzazi.

Daktari wa mwanadada huyo amemwambia Kim “huenda ikawa ni mwisho wa uzazi kwako kwani umegundulika na tatizo katika mfumo wa uzazi”. Kim alishauriwa na daktari huyo kufanyiwa upasuaji kuondoa tatizo hilo kama anataka kupata mototo mwingine.
Baada ya taarifa hizo Kim Kardashian alionekana dhahiri amechanganyikiwa huku akimpigia simu mumewe Kanye West taarifa hiyo ya Kushtua.
Kanye West na Kim Kardashian ni mume na mke wenye mototo mmoja aitwaye North, na huenda wasipate mototo mwingine tena wasipofanyia ufumbuzi tatizo hilo.

Popular Posts