Manchester City kumenyana na Crystal Palace

Mkufunzi wa kilabu ya Crystal Palace Alan Perdew hana majeruhi mapya wakati timu yake inapojiandaa kukabiliana na mabingwa wa ligi ya Uingereza Manchester City siku ya jumatatu.

Mile Jedinak anakamilisha marufuku huku Marouane Chamakh,Fraizer Campbell na Jordon Mutch wakisalia nje.
Yaya Toure aliikosa mechi ya ushindi dhidi ya West Brom wiki moja iliopita na jeraha la mguu lakini sasa amepona baada ya kuichezea Ivory Coast.
James Milner anatarajiwa kucheza licha kusumbuliwa na jeraha la goti katika wiki za hivi karibuni.

Popular Posts