NYOTA WA MAREKANI, NIGERIA AMBAO PIA NI WAJASIRIAMALI

LICHA ya wasanii nyota wa filamu wa Hollywood nchini Marekani kuingiza fedha nyingi kutokana na kuigiza na kudhaminiwa na makampuni makubwa, waigizaji wa Nigeria waliochini ya Nollywood, mambo yao hayaendi vizuri kama wanavyotaka.

Pamoja na kupata mafanikio makubwa katika kuigiza, waigizaji wa Marekani wamejiingiza katika sanaa nyingine nyingi kama yale ya fasheni za mavazi ambako wameingiza mkwanja mkubwa.
Nyota ambao wanaingiza mkwanja mkubwa kila mwaka katika anga hizo, kwa mujibu wa gazeti la Forbes ni pamoja na Nicole Richie ambayo imemwingizia Dola milioni 2, Rachel Zoe Collection (milioni 20), Justin Timberlake na rafiki yake Trace Ayala (milioni 50), Gwen Stefani (milioni 90) na . Victoria Beckham milioni 95) alizovuna mnamo mwaka 2011 peke yake.
Wengine ni P. Diddy na kampuni lake la Sean John ambalo humwingizia Dola milioni 250 kwa mwaka,  Jay-Z (milioni 700 kwa mwaka), Jessica Simpson (Dola milioni 750), Kimora Lee Simmons (milioni 800), Ashley na  Mary-Kate Olsen (Bilioni 1)  Beyonce (Dola 450), na Kardashian (milioni 300), Jennifer Lopez (milioni 300).
Jay-Z.
Katika kufuata nyayo za nyote hao, waigizaji wa Nigeria nao wamejikita katika ujasiriamali kwani hali ya uchumi katika nchi hiyo inawafanya wasipate kipate kizuri.  Isitoshe, nao wanataka kuishi maisha ya anasa na ndiyo maana wanawekeza katika fani mbalimbali za kijasiriamali na baadhi yao kujikita katika siasa.
Waigizaji maarufu wa nchi hiyo ambao wamejikita katika ujasiriamali ni pamoja na Dapo Oyebanji anayajulikana kama  D’Banj.  Yeye ni Mtendaji Mkuu wa kampuni la  Koko Holdings. Genevieve Nnaji ana mradi wa fasheni ya mavazi ya kike uitwao  St. Genevieve.
Kate Henshaw  ambaye pamoja na umaarufu katika uigizaji, ni mtunzi wa vitabu, modo wa mavazi, amewekeza kwenye masuala ya ardhi na nyumba na ana kituo cha mazoezi na kujenga afya.  Mbali na hayo, pia ameingia katika siasa.  Mwanamuziki  Tuface Idibia naye ana klabu moja maarufu ya usiku eneo la Festac Town jijini Lagos.
D’Banj.
Ebube Nwagbo  ni mmiliki mkuu wa kampuni la Posh Hair, wakati  Tonto Dike ana saluni jijini  Lagos. Waigizaji Joy Egbunu na Oby Okafor wana miradi ya huduma za chakula ambapo Oby Okafor ni mkuu wa kampuni la Coded Falour ambapo Joy Egbunu ni mmiliki wa kampuni la vyakula la  Jeez Cusine.
Mwigizaji Dayo Amusa ni mmiliki wa kampuni la  Payday Montessori Creche jijini Lagos na Ibadan mbali na miradi ya fasheni anayoendesha.  Rafiki yake Iyabo Ojo ni mwasisi wa kampuni la urembo la Fespris World jijini Ikeja.
Wajasiriamali wengine ni Bukky Wright aliye na saluni ya urembo, Susan Maxwell mwenye kliniki ya urembo ambapo  mchekeshaji Tee A  na mgahawa, na Ayo Makun, ajulikanaye kama AY, ana hoteli jijini Lagos, ambapo, Seyi Law naye ana hoteli iitwayo  Xcess Lounge eneo la Ikorodu, Lagos.
Genevieve Nnaji.
Wasanii wengine ni  Chidi Mokeme, Bimbo Thomas, KCEE, na  Dayo Adeneye ajulikanaye kama D1,  Laide Bakare,  Obesere, Ayuba, Saidi Osupa, Susan Maxwell, Halima Abubakar, Mercy Aigbe na wengine wengi.
Chidi Mokeme ana kituo cha fasheni eneo la Lekki, Lagos. IT anafanya ujasiriamali wa bidhaa aina nyingi ndani na nje ya Nigeria, ambapo Mercy Aigbe ana kampuni la urembo jijini Lagos na rafiki yake Fathia Balogun ana duka la vileo huko Abeokuta.
Mwigizaji Bimbo Thomas ana biashara ya bidhaa za fasheni wakati Halima Abubakar anajishughulisha na kilimo.Kcee amejikita katika biashara ya mafuta na fesi ambapo  Saidi Osupa na Obesere wanafanya biashara mbalimbali.  Dayo Adeneye na Adewale Ayuba wana hoteli kadhaa jijini Lagos.

Popular Posts