TIKETI ZA 'MAY-PAC
Tiketi za mpambano wa ndondi wa kukata na shoka kati ya Floyd Mayweather na Manny Pacquiao katika dimba la MGM Grand Garden Arena
utakaopigwa tarehe 2 Mei zitaanza kuuzwa leo saa nne usiku saa za Afrika Mashariki.
Kwa wanaotaka kununua bei ya tiketi hizo ni kama ifuatavyo- kutegemea na eneo utakaloketi: Dola 7,500, dola 5,000, dola 3,500, dola 2,500, dola 1,500 na dola 1,000. Masharti -si zaidi ya tiketi nne kwa nyumba moja.