Wanamitindo wembamba wapigwa marufuku
Bunge la Ufaransa limeidhinisha sheria inayopiga marufuku tabia ya makampuni ya wanamitindo nchini humo kutumia wasichana waonesha mitindo walio wembamba kupita kiasi.
Sasa itabidi wanamitindo wembamba kuonyesha kuwa wanauzito wa viwango vinavyokubaliwa kiafya.
Mawakala wa wanamitindo watakaokiuka viwango vilivyowekwa watapigwa faini huku wakuu wa makampuni husika nao huenda wakakabiliwa na vifungo vya hadi miezi 6.
Pia sheria imepitishwa inayopendekeza hatua kuchukuliwa dhidi ya mitandao inayopendelea kuonyesha picha za wasichana walio wembamba kiasi cha kudhoofisha kiafya.