Yanga yaibamiza Coastal Union 8-0
Yanga sasa hii sifa, katika kile kinachoonekana kutoa onyo, imeifunga timu ya Coastal Union 8-0 katika mechi ya ligi kuu Tanzania Bara .
Ushindi huo ni kama tishio pia kwa vigogo wa Tunisia, Etoile du Sahel, ambao siku za usoni watakutana katika kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora.
hadi mapumziko, Yanga ilikuwa inaongoza 3-0 na mvua nyingine ya magoli ilikuwa kipindi cha pili, ambapo Amisi Tambwe alifunga magoli 4, huku Simon Msuva, Salem Telela na Mliberia Kpah Sherman wakiona nyavu pia.
Ushindi huo umeifanya Yanga kuongoza ligi ikiwa na pointing 43, ikiwa ni pigo kwa mabingwa watetezi, Azam , ambao leo pia wametoka share ya 1-1 na Mbeya City uwanja wao wa nyumbani na kubaki nafasi ya pili wakiwa na pointi 37