TP Mazembe wakubali Sammata kuuzwa

Samatta alishindwa kujiunga na CSK Moscow wakati wa dirisha dogo la usajili mwezi Januari mwaka huu kutokana na kupata majeraha

WAKALA wa mshambuliaji Mbwana Samatta wa TP Mazembe, Jamal Kasongo amesema, amefanya mazungumzo na mmiliki wa klabu hiyo Moise Katumbi kujadili juu ya kuuzwa kwa Samatta barani Ulaya.
Kasongo ameiambia Goal, mazungumzo kuhusu mshambuliaji huyo kuuzwa kwenye majira ya kiangazi ni mkubwa kutokana na mmiliki huyo wa TP Mazembe kuridhia kwasababu anaweza kupoteza pesa nyingi endapo atakataa na Samatta anamaliza mkataba wake wa kuichezea timu hiyo Aprili 2016.
“Katumbi ameridhia baada ya hivi karibuni kukutana naye na kuzungumza kuhusu mstakabali wa Mbwana Samatta na huu ndiyo muda pekee kwa Katumbi kutengeneza pesa ni majira ya kiangazi mwaka huu au majira ya baridi mwezi Januari mwakani, akishindwa hapo mwezi wa nne mwakani Mbwana atakuwa mchezaji huru, ataondoka bure,”amesema Katumbi.
Samatta alishindwa kujiunga na CSK Moscow wakati wa dirisha dogo la usajili mwezi Januari mwaka huu kutokana na kupata majeraha siku moja kabla ya kucheza mechi ya kirafiki ambayo maamuzi yangetoka moja kwa moja katika siku tatu alizofanya majaribio CSK Moscow alicheza vizuri na alifunga magoli matatu lakini alishindwa kucheza mechi ya kirafiki baada ya kuumia kifundo cha mguu.

Popular Posts