Kamati ya Utendaji TFF yasitisha ajira ya Nooij




Mart Nooij amekua hana matokeo yakuridhisha na Timu ya Taifa ikiwemo vipigo viwili mfululizo dhidi ya Misri na Uganda


Kocha wa Taifa Stars Mart Nooij ajira yake imesitishwa na Kamati ya utendaji baada ya kutoridhishwa na matokeo ya timu.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari inasema “Kamati ya utendaji ya Shirikishi la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Katika kikao chake cha pamoja na mambo mengine ilipitia mwenendo wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mchezo kati ya Tanzania na Uganda, kama sehemu ya tathmin ya mwenendo wa timu”.
Taarifa hio imeendelea kusema yafuatayo
“Kamati ya utendaji kwa kauli moja imeamua yafuatayo:
1.Ajira ya Kocha Mkuu Maart Nooij inasitishwa mara moja kuanzia  tarehe 21/June/2015.
2.Benchi lote la ufundi la Taifa stars limevunjwa kuanzia tarehe 21/06/2015.
3.Uongozi wa TFF utatangaza punde benchi jipya la ufundi la timu ya Taifa.”
Mart Nooij amekua hana matokeo yakuridhisha na Timu ya Taifa ikiwemo vipigo viwili mfululizo dhidi ya Misri na Uganda.

Popular Posts