Skip to main content

Hamisi Kiiza asaini miaka miwili Simba

Kiiza amesaini mkataba baada ya kufuzu vipimo vya afya alivyo fanyiwa na madaktari wa timu hiyo kwenye Hospital ya michezo iliyopo Msasani

HATIMAYE mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Uganda Hamisi Kiiza amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea klabu ya Simba ya Dar es Salaam Tanzania.
Kiiza amesaini mkataba baada ya kufuzu vipimo vya afya alivyo fanyiwa na madaktari wa timu hiyo kwenye Hospital ya michezo iliyopo Msasani na baada ya hapo alisaini mkataba na sasa ni mali ya Simba.
Baada ya kusaini Kiiza ameiambia Goal amekuja kufanya kazi na Simba na kuipa mafanikio kama alivyo fanya akiwa na Yanga na kuwataka mashabiki na wanachama wa timu hiyo kumpa sapoti ili aweze kufanikisha malengo yake ya kuirudisha Simba kwenye ubora iliokuwa nao siku za nyuma.

Popular Posts