TETESI ZA USAJILI



1.Chelsea wamemsajili kipa wa Stoke City Asmir Begovic kwa kitita kinachodhaniwa kuwa pauni milioni 8. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Bosnia-Hercegovina, 28, amesaini mkataba wa miaka minne Stamford Bridge.



2.Kiungo wa Southampton Morgan Schneiderlin anafaya vipimo vya afya kabla ya kukamilisha uhamisho wake unaodhaniwa kuwa wa pauni milioni 25 kwenda Manchester United.

3.Liverpool wamekubaliana na Manchester City kuhusiana na uhamisho wa pauni milioni 49 wa Raheem Sterling.
Uhamisho wa winga huyo, 20, sasa utategemea makubaliano ya mkataba na vipimo vya afya.
Sterling aliomba kuondoka Anfield, huku dau la City likikataliwa mara mbili mwezi Juni.
Streling, ambaye atakuwa mchezaji aghali zaidi kutoka England, mkataba wake unaisha mwaka 2017, lakini aligoma kuuongeza baada ya kukataa mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki. 
Siku ya Jumamosi, Sterling alitajwa katika kikosi cha wachezaji 30 wa Liverpool wanaokwenda Thailand, Australia na Malaysia, lakini baadaye jina lake liliondolewa.

Popular Posts