Barca, Bayern zapeta
Vigogo wa soka barani ulaya Barcelona, na Bayern Munich, wameishindi katika michezo yao ya pili ya klabu bingwa ulaya.
Barcelona, waliwachapa Bayern 04 Leverkusen, kwa mabao 2-1 mabao ya Barca, yakifugwa na Luis Suárez na Sergi Roberto, huku la Bayern likifugwa na Kyriakos Papadopoulos.
Bayern munich, wakawalaza Dinamo Zagreb, kwa kuwachapa 5-0 mshambuliaji Robert Lewandowski, akifunga mabao matatu huku mengine yakifugwa na Douglas Costa, na Mario Gotze.
Chelsea, wakicheza ugenini huko nchini Ureno, wakakubali kichapo cha mabao 2-1 mabao ya Porto yakiwekwa kambani na Brás André na Maicon, huku lile la kufutia machozi la Chelsea, likifugwa na Mbrazil Willian.
Washika bunduki wa Arsenal wakiwa katika uwanja wao wa Emirate wakachabangwa kwa mabao 3-2Olympiakos,
Matokeoa mengine ya michezo ya klabu bingwa ulaya
BATE Bor 3 – 2 Roma
Maccabi Tel Aviv 0 - 2Dynamo Kiev
Lyon 0 – 1 Valencia
Zenit St P 2 – 1 KAA Gent