Benitez nje Real Madrid
Uongozi wa klabu ya Real Madrid umemtimua kocha wake Rafael Benitez ambaye ana Miezi 7 tu katika Mkataba wake wa Miaka Mitatu.
Sasa nafasi yake imechukuliwa na mchezaji mkongwe mfaransa Zinedine Zidane ambaye awali alikuwa Kocha wa Kikosi B cha Real Madrid .
Hii inatokana na matokeo mabaya kwa timu hiyo, ambapo ilitoka Sare 2-2 na Valencia, katika Mechi ya La Liga, Sare ambayo imewaacha Vigogo hao nafasi ya 3 wakiwa nyuma ya Atletico Madrid kwa pointi 4.
Tangu atue Madrid, Benitez amekuwa si kipenzi cha Mashabiki wa Klabu hiyo, baada ya kufungwa bao 4-0 kwenye mechi ya El Clasico Mwezi Novemba na Mahasimu wao Barcelona, pia kutupwa nje ya michuano ya Copa del Rey.