HUU NDIO UBORA WA NYOTA YA RASHFORD
Kinda la Manchester United Marcus Rashford amesaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia Old Trafford hadi June 2020
Alifunga mara mbili kwenye
Rashford alichaguliwa kujiunga na kikosi cha England cha wachezaji 26 kwa ajili ya michuano ya Euro 2016 na akafunga wakati akiichezea timu ya taifa kwa mara ya kwanza dhidi ya Australia siku ya Ijumaa.
“Nimefurahi kupata fursa ya kuendelea kuthibitisha uwezo wangu”, alisema baada ya kusaini mkataba mpya.
“Kupata nafasi ya kucheza kwenye klabu kubwa duniani inamaanisha kilakitu kwangu na kwa familia yangu.”
Kutana na mambo nane yaliyolipaisha jina la Marcus Rashford, hata angekuwa nani lazima angetoa mkataba kwa kinda huyu ili kuendelea kupata huduma yake kwa muda mrefu.
February 25: Anthony Martial anaumia wakati wa kufanya warm-up kuelekea mchezo wa Europa League mchezo dhidi ya Midtjylland. Rashford akapata nafasi kwenye kikosi cha kwanza na akafunga bao mbili kwenye ushindi wa magoli 5-1
February 28: Rashford akapiga tena bao mbili dhidi ya Arsenal kwenye ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Arsenal ikiwa ni mchezo wake wa kwanza wa Premier League, mechi hiyo ilichezwa uwanja wa Old Trafford.
March 20: Akiwa amepita kwenye kipindi cha mwezi mmoja bila kufunga goli, alifunga bao kwenye mchezo wa Manchester derby dhidi ya Manchester City.
March 27: Alicheza mechi yake ya kwanza kwenye kikosi cha England cha U20 lakini the Young Lions kilipoteza mchezo huo kwa magoli 2-1 dhidi ya Canada.
April 13: Alipika bao kwenye mchezo wa nusu fainali ya FA Cup na kuisaidia timu yake kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya West Ham.
April 16: Bao lake liliishusha kwenye ligi Aston Villa wakati United ikipata ushindi wa bao 1-0 kwenye uwanja wa Old Trafford.
May 16: Alitajwa kwenye kikosi cha England kitakachoshiriki michuano ya Euro 2016.
May 27: Alicheza mechi yake ya kwanza kwenye kikosi cha wakubwa cha England na kufunga bao baada ya dakika tatu kwenye mchezo wake wa kwanza akiwa timu ya taifa ya wakubwa.