KAMA ULIMISS UTEUZI ULIOFANYWA JANA NA RAIS JOHN P. MAGUFULI
Rais Dkt. John Magufuli amemteua Jaji Shabani Lila kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huo Jaji Lila alikuwa Jaji Kiongozi
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Anne Makinda kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya -NHIF.
Makinda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Ali Mchumo na uteuzi wake umeanza Mei 25 mwaka huu.
Halkadhalika Rais Magufuli amemteua Profesa Apollinaria Pereka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam - DIT. Profesa Pereka anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Profesa Fredrick Mwanuzi ambaye amemaliza muda wake.
Profesa Pereka ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo -SUA.
Uteuzi wake umeanza tarehe 30 Mei, 2016.
30 May 2016