Mbwana Samatta kucheza Europa league

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ameingoza KRC Genk kufuzu kucheza Ligi ya Europa baada ya kuichapa Sporting Charleroi kwa mabao 5­-1 na kushinda kwa jumla ya mabao 5-­3.


Kulingana na gazeti la Mwananchi, Samatta, ambaye katika mchezo wa kwanza walionyukwa 2­0 alianzia benchi, jana aliaminiwa kuanza mchezo huo na kocha wake Peter Maes, akicheza pamoja na Nikos Karelis katika safu ya bora ya ushambuliaji.
Katika mchezo huo, Samatta alifunga bao moja na kutegeneza mengine mawili yaliyofungwa na Karelis ambaye alifunga magoli matatu katika mchezo huo, na Sandy Walsh akifunga bao moja kabla ya Sporting Charleroi kupata bao la kufutia machozi lililofungwa na Jeremy Perbet.
Kulingana na Mwananchi,Genk, ikicheza kwenye uga wake wa nyumbani wa Cristal Arena ilianza mchezo kwa kasi na dakika 16, ilipata penalti baada ya Samatta kuangushwa kwenye eneo la hatari na kipa Nicolas Penneteau, ambaye alipewa kadi nyekundu.
Samata aliwainua mashabiki wa Genk kwa kupachika bao la pili akiungamisha mpira uliotemwa na kipa wa Sporting, Penneteau katika dakika 27, kabla ya Sporting Charleroi kupata bao dakika 40 lililofungwa na Jeremy Perbet na kuifanya timu hizo kwenda mapumziko ikiongoza kwa mabao 2­1.
Genk ilianza kipindi cha pili kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la tatu lililofungwa na Sandy Walsh kulingana na mwananchi.
Ushirikiano mzuri baina ya Samatta na Karelis ulisaidia kupatikana kwa bao la nne wakati Mtanzania huyo alipokimbia na mpira na kuwa katika nafasi mbili za kutoa pasi kwa Bailey au Karelis.

Popular Posts