Jose Mourinho atupa jikenmbe kwa Pep Guardiola
Jose Mourinho amesema kamwe hatathubutu kupoteza muda wake kumwangalia Pep Guardiola pekee kwenye ligi ya England msimu ujao, kwasababu anaamini akifanya hivyo, basi ataruhusu timu nyingine kuchukua ubingwa.
Mourinho, ambaye aliteuliwa kocha wa Manchester United wiki iliyopita anakabiliwa na mtihani mgumu mbeleni kutokana na uwepo wa hasimu wake mkubwa Pep Guardiola ambaye atakuwa akiinoa Manchester City ambao ni mahasimu wakubwa wa Manchester United.
Ikumbukwe tu vita ya Guardiola na Mourinho ilianza nchini Hispania wakati huo Mourinho akiinoa Real Madrid na Guardiola akiinoa FC Barcelona.
Licha ya uhasimu mkubwa walionao kutokana na historia yao, Mourinho amesisitiza kwamba hataendekeza jambo hilo katika maisha yake mapya ya ukocha katika klabu ya Manchester United
Akiongea wakati akiwa Lisbon University, Mourinho alisema: “Uzoefu wangu hauniruhusu mimi kuwa innocent (mtu asjiye na hatia).
“Nilikuwa na Guardiola kwa miaka miwili La Liga ambapo ilikuwa ama mimi au yeye ndiyo tulikuwa tuna nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa. Lakini hapa kama nikisema nimwangilie tu yeye, basi timu nyingine zitanipiku na kuchukua ubingwa”.