katy perry adukuliwa mtandaoni

Katy Perry ndio mtu aliye na mashabiki wengi wanaomfuata katika mtandao wa Twitter lakini hata yeye hakusazwa na wahalifu wa mitandaoni.
Akaunti yake ilivamiwa na wahalifu wa mtandaoni
huku msanii huyo akituma ujumbe usio wa kawaida kwa wafuasi wake wapatao takriban milioni 89.
Ujumbe mmoja ulitumwa kwa mpinzani wake mkuu katika muziki wa Pop Taylor Swift akimwambia kwamba anamuenzi.
Image captionKaty Perry
Ujumbe huo hatahivyo ulifutiliwa mbali na nywila yake kubadilishwa.
Ujumbe huo wa Twitter ulishirikisha maneno ya ubaguzi wa rangi na ombi la kufuata akaunti nynegine ya Twitter.
Kaunti hiyo pia ilituma ujumbe wa Twitter wa nyimbo kwenye mtandao wa SoundCloud ambayo inaaminika kuwa nyimbo ya Katy Perry kwa jina Witness ambayo haijatolewa.
Image captionKaty Perry
Hatahivyo wimbo huo umeondolewa pamoja na ujumbe uliotumwa,lakini picha za ujumbe huo wa Twitter zilikuwa tayari zimesambazwa mtandaoni.
bbcswahili chanzo

Popular Posts