taarifa ya polisi tanga kuhusu watu 8 waliouawa

Kamanda wa Polisi Tanga Leonard Paul amesema ilikua saa saba usiku wa kuamkia May 31 2016 kwenye kitongoji cha Kibatini kata ya Mzizima wilaya ya Tanga umbali wa kilomita 40 – 45 kutoka Tanga mjini sehemu ambako kuna msitu kabla ya
kukuta nyumba zipatazo 20 Majambazi walivamia wakiwa na visu na mapanga.
Walivamia nyumba tatu na kuua watu wote hao 8 kwa kuwakata mapanga shingoni pia waliiba biskuti, mchele na sukari na baada ya wizi huo walitokomea msituni maeneo ya Amboni ambayo yanazungukwa na kitongoji hicho cha Kibatini.
Kwa kumalizia Kamanda Leonard Paul amesema >>> ‘Jeshi la Polisi linashirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuwasaka wauaji hao, hakika tutawakamata….. ndugu Waandishi nisingependa kusema mengi sasa kwani yanaweza kuingilia upelelezi wa shauri hili’

Popular Posts