wema aanza kuona manufaa ya app.

Muigizaji wa kike katika kiwanda cha filamu Tanzania, Wema Abraham Sepetu, amesema tayari ameanza kuiona faida kifedha ya huduma ya ‘App’ yake mtandaoni aliyoizindua majuma kadhaa nyuma.

Akiongea kupitia kipindi cha Kubamba cha Times Fm, Wema amedai kwa sasa anaangalia kwa ukaribu zaidi biashara zake na ndio maana asikiki kwenye mambo yasiyo na faida kwake.
“Na focus kwenye kazi kama Magufuli anavyosema, App yangu nashukuru nimeona mapokeo na imeanza kuniingizia fedha nzuri tu” Alisema.

chANZO TIMES FM

Popular Posts